Makala

Thawabu kwa atakayetawadha vyema kipindi cha baridi kali akiwa anapata tabu.

User Rating: 5 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Active
 

.


Imepokelewa kutoka kwa Jābir bin 'Abdillāh (Allāh amridhie) amesema:

Amesema Mtume wa Allāh ﷺ:

"Hivi nisikujuzeni juu ya yale ambayo kwayo Allāh hufuta makosa na kusamehe madhambi?

Wakasema: Tujuze ewe Mtume wa Allāh!

Akasema:

"Ni kutawadha vyema wakati wa machukizo, na kukithirisha hatua kuelekea Msikitini, na kusubiri swala baada ya swala."


رواه ابن حبان في "صحيحه" (١٠٣٦).
وأصله عند مسلم (٢٥١).

Ameipokea Ibn Hibbān katika "Sahihi" take (1036), na asili yake ipo katika "Sahihi" Muslim.

 

Faida za Hadithi


1. Ukamilifu wa Dini ya Kiislamu na ubora wake mbele ya Dini nyingine.

2. Anatakiwa Muislamu ajitahidi kujifunza sifa ya Udhu wa Mtume Muhammad ﷺ kwani hatoupata ujira huu ila aliyetawadha kama alivyotawadha yeye ﷺ.

3. Kutawadha wakati wa machukizo mfano wake ni kutawadha wakati wa baridi kali na mtawadhaji akashindwa kuyapoza maji yake hayo, au kuteseka katika kuyatafuta maji yaliyo mbali na mfano wake. Na hadithi haiashirii kwa mbali wala kwa karibu kwamba mtawadhaji ajitese kwa makusudi kwa kutafuta maji ya barafu wakati maji ya kawaida yapo.

4. Bishara njema kwa wanaoishi mbali na Misikiti ambao hupiga hatua kutoka majumbani mwao huko mpaka Misikitini. Na imekuja hadith Mtume ﷺ anawaambia Baniy Salimah:

"Lazimianeni na majumba yenu kwani hatua zenu zitaandikwa."

Ni pale walipodhamiria kuhamia jirani na Msikiti wake ﷺ.

Na hadithi ameipokea Muslim kutoka kwa Jābir.

Inajulisha juu ya fadhila nyingi azipatazo anayekaa mbali na Msikiti kwa sababu ya wingi wa hatua zake kuelekea Msikitini. Pia kutoka kwa Abū Mūsaa (Allāh amridhie) kutoka kwa Mtume wa Allāh ﷺ amesema

"Hakika mwenye ujira mkubwa sana katika watu wanaoiendea swala ni yule anayetokea mbali."

Bukhar na Muslim.


5. Malipo makubwa kwa anayesubiri swala baada ya swala. Na hili lipo katika sura nyingi ambazo wanazitaja Wanazuoni wetu wa Kiislamu ikiwemo sura ya;

- aliyeswali sunnah akasubiri faradhi, au faradhi akasubiri sunnah, au faradhi akasubiri faradhi nyingine akiwa ndani ya Msikiti.

- Ni yule aliyeswali swala na bado moyo wake ukawa umefungamana na ngojeo la swala nyingine hata kama atatoka Msikitini.


Na kwa yule atakayebaki Msikitini ima kwa kufanya adhkari kama vile kusoma Qur'an au kusoma elimu na kusikiliza Darsa mpaka akafikiwa na wakati wa swala nyingine, muda wake wote huo alioukaa ataaandikiwa kuwa yupo ndani ya swala.


Mtarjim: duaatsalaftz.net
Muhusika: duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 09/07/2020

Nasaha

©2020 uaat Salaf Tanzania - . All Rights Reserved. Designed By Wajanjatech.Com

Search