Makala

Ukombozi Wa (Allāh) Mneemeshaji Katika Kumjibu Mshia Muovu – 02

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
 
Neno la Mchapishaji limenena:
“Maadui wa Uislamu siku zote hutumia hitilafu za madhehebu ili kuwafitinisha Waislamu wasiwe na umoja. Kwa bahati mbaya sana, mbinu
hii imefanikiwa sana kwa kiasi fulani.”

Majibu Yetu:

Hii ni talbisi yenu ya kwanza kwa Waislamu, kutaka kuiaminisha jamii ya Waislamu kuwa eti na nyinyi (shia) ni miongoni mwao! Ilhali baina ya Waislamu na nyinyi kuna mtengano mkubwa na tofauti kubwa kama ile iliyopo baina ya samāi na ardhi, bali baina ya mashariki na magharibi, na hilo ni kwa sababu ya kutofautiana kwa Itikadi za Waislamu na itikadi zenu.
Itikadi za Waislamu ni kumpwekesha Allāh na kumtakasia Ibada Zake, na kwamba haifai kuombwa pamoja na Allāh mwengine yeyote, si Malaika aliyekurubishwa (kama vile Jibriil), wala Nabii aliyepewa Utume (kama vile Muhammad swalla Llāhu alayhi wasallam), wote hao haifai kuwaomba badala ya Allāh.
Na katika Itikadi za Waislamu ni kuwa hakuna ajuaye ghaibu isipokuwa Allāh Pekee.
Na miongoni mwa Itikadi za Waislamu ni kuwapenda Maswahaba wa Mtukufu Mtume Muhammadﷺ, na kuwatakia radhi za Allāh ziwe juu yao, na kuamini kuwa wao ni bora ya viumbe wa Allāh baada ya Mitume na Manabii (‘alayhimus-salaam). Na kwamba wa kwanza wao katika ubora na fadhila ni Abūbakr Al-Swiddiiq, kisha ‘Umar Al-Fāruuq, kisha ‘Uthmaan bin ‘Affān, kisha ‘Aliyy bin Abiy-Twalib (Allāh awaridhie wote!). Na shia wapo kinyume na hayo yote, hivyo haitofaa kuwahesabu kuwa ni Waislamu, kama ambavyo haitofaa kuwaingiza katika orodha ya Waislamu mayahudi na manaswara, kwa kuwa Itikadi zao ni Tofauti na Itikadi za Waislamu, basi vivyo hivyo mashia kwa Waislamu.
Shia mmekufurishwa na Maimamu wa Ahlus-Sunnah wakubwa waliosoma wakabobea, mfano Imam Mālik bin Anas (Allāh amrahamu), ambaye ni Sheikh wa Imam Shaafi’iy (Allāh amrahamu), na hakuna aliyempinga Imam Maalik katika shauri lake hilo la kuwakufurisheni, bali wamemuunga mkono katika hilo idadi kubwa ya ‘Ulamaa na Wanazuoni.
Tazama: Tafsiir ya Ibn Kathiir (Mwishoni wa Suuratul-Fat’h).
Huyu hapa Imam Al-Qurtubiy anamuunga mkono Mālik, Imam wa Dārul-Hijrat;
Amesema Al-Imām Al-Qurtubiy (Allāh amrahamu):
“Na kwa hakika amepatia (Imam) Mālik, katika maneno yake (hayo dhidi ya ukafiri wa shia), na amesibu katika tafsiri yake hiyo…”
Rejea Tafsiir Al-Qurtubiy.
Hivyo shia jijueni kuwa lakum-diinukum walil-Muslmiin Diin.
Allāh amrehemu Imam wetu wa madhehebu (Imam Shaafiy) pale aliposema kuhusu Fatawa za Imam Maalik kule Madinah, alisema hivi:
“Pindi wanapotajwa Wanazuoni basi (Imam) Mālik ni nyota.”
Na katika methali iliyoshuhurika husema:
“Haitolewi fat’wa na yeyote ilhali Mālik bado yupo Madinah.”
Na huyo ndiye aliyekukufurusheni.
Na ushia si madhehebu, bali ushia ni Dini yenye kujitegemea yenye kutofautiana na Dini ya Kiislamu katika Misingi yake na Matawi, Kanuni zake za Istinbātwi na Masaadir ya kujenga hoja, ni Dini iliyo na taratibu zake na itikadi zake, kama vile dini zingine.
Muache kuwazeveza Waislamu na kuwachanganya kwa talbiis zenu kuwa eti nanyi ni Waislamu na mnayo madhehebu yenu ambayo ni ya tano juu ya zile nne za Waislamu zilizoshuhurika:
 • Madh-hab Shāfi’iy
 • Madh-hab Hanbaliy
 • Madh-hab Hanafiy
 • Madh-hab Māliky
Na ya kwenu inatiwa:
 • Madh-hab Ja’fariyy!!!!
Na madhehebu yao hii imepitishwa kwa madai yao na Sheikh Mahmuud Shaltuut aliyekuwa Sheikh mkuu wa chuo kikuu cha Azhar kule Misri.
Na kwamba katika aliyoyasema juu ya kuipitisha kwake madhehebu hiyo:
“Hakika madhehebu ya Ja’fariyyah inayotambulikana kwa jina la madhehebu ya shia Imaamiyyah Ithnay-Ashariyyah, ni madhehebu inayofaa kuifuata kisharia, kama zilivyo madhehebu nyingine za Ahlus-Sunnah, hivyo inatakikana kwa Waislamu walijue hilo, na wajiepushe kabisa na suala la ubaguzi pasi na haki, kubagua madhehebu maalumu..”
Rejea: Fikihi kwa mujibu wa madhehebu tano UK 8.
Na hili kama limethibiti haliwi mbali kwa mtu mithili ya Shaltuut kulipitisha na kulijuzisha kwani watarajia nini ndugu Msomaji kwa Sheikh mithili ya huyu Mahmuud Shaltuut aliyekuwa Sheikh mkuu wa chuo kikuu cha Azhar ambaye alishawahi kuhalalisha Riba, na kupinga juu ya kurejea kwa Nabii Issa? Ikiwa aliweza kukinzana na Mola wake aliyeharamisha Riba na kwenda kinyume na Mtume wake aliyemlaani mla Riba, mwandishi wake, na mashahidi wake wawili!? Hivi kutakuwa na ajabu gani tena kwake mpaka tutaharuki sisi Waislamu Ahlus-Sunnah Waljamā’ah kwa fat’wa hiyo ya Shaltuut mwenye balaa hizo?
Shaltuut ambaye wenzake wamemkataa juu fat’wa zake hizo.
Na utapingaje ndugu Msomaji kama utaambiwa kuwa Shaltuut naye alipewa bahasha za kaki!?
Kwa sababu katika wakati wake kulikuwa na mvutano mkubwa sana baina ya shia na Waislamu pamoja na Masheikh wa Azhar, mpaka katika kuleta islahi na suluhu ikaanzishwa kamati ya kusimamia mgogoro huo, na Shaltuut alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, ndipo katika jitihada za kuleta umoja baina ya Sunniy na shia (umoja batili), wakaongeza shia madhehebu hiyo wanayoiita ya tano ili nayo ipitishwe na kamati hiyo ambayo Shaltuut ni katika wajumbe wake, na isomeshwe katika chuo kikuu cha Azhar, lakini kwa kuwa simba haendi hija, na hata ukimpeleka hija akirudi akiwaona swara na sungura ute utamtoka mwishowe ni kuharibu hija yake kwa kuwashambulia na kuwavamia, pamoja na harakati zote hizo za kujitahidi kuleta umoja baina ya pande mbili hizo (umoja usiowezekana), mara kituko kimoja cha kishia kiitwacho (Abdul-Husayn Sharafud-Diin Al-Mūsawiy) kikatunga kitabu kipindi cha harakati hizo na kukiita kitabu chake hicho kwa jina la Swahaba Mtukufu “Abū Hurayrah” (Allāh amridhie), kituko hicho cha shia kikamtusi matusi ya nguoni Abū Hurayrah (wetu), na mwisho kikamkufurisha na kumwita Swahaba huyu kuwa ni MNAFIKI.
Na jinsi walivyokuwa hawana haya wala kujua vibaya, kitabu hicho kinachomkufurisha Abū Hurayrah (Allāh Amridhie) hakikubaki kuwa ni fumbo kwa kubakishwa katika lugha ya kiarabu iliyotumiwa na mwandishi wake ili jamii ya Waislamu waswahili wasijue kinachoendelea kama wanavyoficha baadhi ya mambo yao machafu ya kujuzisha kuwaingilia wanawake kinyume na maumbile na kuchezea vinyesi , bali wamekifanyia tarjamah kwa lugha ya kiswahili ili mja na muungwana aone ukafiri wa Swahaba Abū Hurayrah (Allāh amridhie).
Je ndugu msomaji umoja utapatikana hapo baina ya Sunniy na shia kama alivyokubali Shaltuut na kuidhinisha madhehebu ya Ja’fariyy isomeshwe katika chuo kikuu cha Azhar?
Ndugu msomaji bila shaka unakumbuka vizuri miaka ile wale akina fulani katika Masheikh walipokuwa wanapigia debe fikra ya Dini mseto kipi kilichotokea!!
Bila shaka waliokuja juu walikuwa wakipinga kuchanganywa Itikadi za Dini ya hawa juu ya Itikadi za Dini ya hawa!
Walikuja juu Waislamu kwa kujua kwao kuwa Dini mbili ni Itikadi mbili na hazikutani mahala pamoja, vivyo hivyo Dini ya ushia na Uislamu.
Hayo ya kamati ya Shaltuut ameyataja Duktuur Mustapha Al-Sibā’iy katika kitabu chake “Al-Sunnāh Wamakaanatuha”.
Na sisi lau tungelikuwepo wakati wa kamati ya Shaltuut tungemuuliza Sheikh huyo wa Azhar wakati wake maswali yafuatayo:
 1.  Anawezaje kuwa Muislamu mwenye kumtusi Abūbakr na ‘Umar (Allāh awaridhie) kwa matusi machafu kabisa? Mbali na kuruhusu madhehebu hiyo ya tano.
 2. Anawezaje kuwa Muislamu mwenye kumtusi mama wa Waumini Āisha mwana wa Abūbakr Al-Swiddiq ambaye ni mke wa Mtukufu Mtume
  Muhammadﷺ? Aliyetakaswa na Allāh kutoka juu ya mbingu saba? Mbali na kuruhusu madhehebu hiyo ya tano.
 3. Anawezaje kuwa Muislamu yule anayewahukumu Maswahaba wa Mtume Muhammadﷺ kuwa wote waliritadi baada ya kufariki Mtume (swalla Llāhu alayhi wasallam) ila wachache tu ambao hawavuki idadi ya vidole vya mkono? Mbali na kuruhusu madhehebu hiyo ya tano.
 4. Anawezaje kuwa Muislamu mwenye kudai kuwa Imam ‘Aliyy hakosei, si yeye tu bali na watoto wake kumi na mmoja, ilhali ‘Ismah ya kukingwa na makosa ipo kwa Mitume na Manabii tu? Mbali na kuruhusu madhehebu hiyo ya tano.
 5. Anawezaje kuwa Muislamu mwenye kuwaomba viumbe waliokufa na waliohai? Mwenyekudai kuwa kufanya hija Karbalaa ni sawa na kuhiji katika nyumba ya Allāh Tukufu? Mbali na kuruhusu madhehebu hiyo ya tano.
 6. Anawezaje kuwa Muislamu mwenyekudai kuwa Malaika mwaminiwa wa Allāh Jibriil (‘Alayhis-Salaam) alifanya khiyana katika kuuleta Utume kwa Muhammadﷺ, badala ya ‘Aliyy? Mbali na kuruhusu madhehebu hiyo ya tano.
 7. Anawezaje kuwa Muislamu mwenyekudai kuwa Mahdy Al-Muntazar atakapotoka kuja duniani atapatikanisha ambayo aliyashindwa
  Muhammadﷺ? Mbali na kuruhusu madhehebu hiyo ya tano.
Madhehebu ya tano (ya shia) haikubaliki.
Madhehebu hiyo yao ya tano wanayolazimisha iingie juu ya madhehebu za Waislamu nne, inayoitwa (Al-Ja’fariyy), imenasibishwa kwa Imam wao Ja’far bin Muhammad (Al-Swādiq), na madhehebu nne za Waislamu zilizoshuhurika zinanasibisishwa kwa Maimamu wanne wa Ahlus-Sunnah
 • Muhammad bin Idriis (Shaafy)
 • Ahmad bin Hanbal Al-Shaybāniy
 • Mālik bin Anas Al-Asbahiy
 • Abū Haniifah Nu’mān bin Thaabit
Allāh awarahamu wote!
Hawa Maimamu hawakuwa Mitume wala Manabii, na wala hawajakingwa kutokana na makosa, kwa maana wanapatia na kukosea, hivyo katika vitabu vyao hakuna salama ya kusalimika na makosa kwani ukamilifu ni wa Allāh, kipindi ambacho madhehebu ya shia ni madhehebu isiyo na kosa hata dogo, kwani madhehebu yao imetokana na Imam aliyekingwa na makosa ambaye hazungumzi kwa matashi yake bali anachokifanya au kukisema ni haki tupu, sasa madhehebu kama hii kuiorodhesha na zile nne za Maimamu ambao hawajakingwa na makosa ni dhulma kubwa.
Cha ajabu ni kuwa madhehebu nne za Waislamu Ahlus-Sunnah zina sanadi ya moja kwa moja kutoka kwa wenyekunasibishiwa madhehebu hizo, mfano ukiizungumzia madhehebu yetu ya Shaafi’iyyah, utakutana na Kitabu ambacho mwandishi wake ni mwenyewe Imam Shaafiy (Allāh amrahamu), na baadhi ya ambayo hayamo kwenye kitabu chake hicho yanayohusu madhehebu hiyo utayapata katika vitabu vya wanafunzi wake Imam huyo, kipindi ambacho hiyo inayoitwa Madhehebu ya Ja’fariyy ni simulizi za watu wa mji wa Kufah kule Iraq ambao wanasimulia ya aliyeishi Madinah (Imam Ja’far), si kitabu cha Imam wao, wala si mwanafunz wa Imam aliyeishi na Imam akaandika aliyoyapata kutoka kwa Imam!!
Na nne zetu ni madhehebu ya kimatawi ya fiqh, ndo maana utaona wametofautiana mitazamo na maono, ama katika upande wa Itikadi wote wapo sawa hawajatofautiana, lakini sisi na nyie shia tumetofautiana katika Usuulul-Iymaan, kama vile mayahudi na manaswara.
Ambacho kinaliwaza ni kuwa alhamdulillah wengi katika Ahlus-Sunnah wameshawajua nyie shia, na Allāh kila panapokucha anafichua yaliyomo mioyoni mwenu kwa kuwatamkisha kwa ndimi zenu yale mliyoyaficha vifuani mwenu miongoni mwa kufru, nifaq na zandaqah.
Na amesema kweli Allāh Mtukufu:

مَّا كَانَ اللَّهُ لِيَذَرَ الْمُؤْمِنِينَ عَلَىٰ مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ ۗ ” آل عمران (١٧٩).

“Haiwi kwa Allāh kuwaacha Waislamu katika hali mliyo nayo mpaka Apambanue wabaya katika wema.”
Al-‘Imrān (179).
Na amesema kweli Amiiril-Mu’miniina ‘Uthmān bin ‘Affān (Allāh amridhie):

ما أسرَّ أحد سريرة إلا أظهرها الله- عز وجل- على صفحات وجهه وفلتات لسانه”.

“Hatoficha mtu siri (nafsini mwake) isipokuwa ataidhihirisha Allāh katika safha za uso wake na mtelezo wa Ulimi wake.”
“Al-Ādābush-Shar-‘Iyyah” (1/136).

 

Mhusika: Al-Akh Abuu Ayman Al-Shiraaziy
Mkusanyaji: http://duaatsalaftz.net/

Nasaha

©2020 uaat Salaf Tanzania - . All Rights Reserved. Designed By Wajanjatech.Com

Search