Je Aliefariki Hali Ya Kuwa Ni Mjamzito Azikwa Na Mtoto Tumboni?


Swali:
assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuh, ni ipi hukumu ya namna ya kumzika mwanamke aliyefariki na ujauzito wake? ninamaaanisha kuwa mama kafariki na mtoto wake ilihali mtoto bado yuko tumboni na
a) mtoto yuko chini ya miez4
b) mtoto ana umri zaidi ya miezi minne
baaraka llahu fiikum
Jawabu:
الحمد لله رب العالمين ، والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء وإمام المرسلين وبعد
وفيكم بارك الله
Ama kuhusu hukumu ya namna ya kumzika mwanamke aliyefariki akiwa na ujauzito wake kwa mujibu wa fat’wa za Ahlul-‘Ilmi kama vile Al-‘Allaamah ‘Abdul-‘Aziiz bin ‘Abdillaah bin Baaz (ALLAAH Amraham!) , anaonelea azikwe kwa hali hiyo hiyo ya ujauzito wake na wala hakuna haja ya kupasuliwa muda wa kuwa amekufa pia mwanae aliye tumboni.
Ama ikihakikiwa kuwa mtoto aliye tumboni yuhai basi atapasuliwa maiti kwa maslahi ya aliye hai.
والله ولي التوفيق .
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 08/11/2016