Je Mtoto Aruhusiwa Kumshawishi Mama Ake Aolewe Baada Ya Baba Yake Kufariki?


Swali:
Assalamu alaikum warahmatullahi wabarakatuh.
Miezi tisa imepita tokea baba yetu afariki, lakini mama yetu tokea alipomaliza eda hajakubali kuolewa licha ya kwamba watu wengi wameshamfuata kwa ajili ya jambo hilo.
Je tunaruhusika kisheria sisi watoto wake kumshawishi kulikubali jambo hilo?.
Jawabu:
Huenda mama bado ana machungu ya kuondokewa na mumewe na anahisi hatopata mume kama huyo tena, au kuna maudhi aliyokua akikumbana nayo ktk ndoa sasa hataki kukutana nayo tena.
Allah anajua zaidi Hakuna ubaya kumnasihi mama yenu kwa njia iliyo nzuri bila kumkosea adabu.
Lakini kama mwenyewe ataamua kukaa bila mume na akawa mwenye kujihifadhi vyema. Basi asilazimishwe kuolewa.
Wabillahit taufiyq.
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 12/10/2016