Kula Chakula Cha Wakwe Ambao Hawajafunga Ndoa


nimeowa mwanamke lakini wakwe zangu awajaowana je inafaa kula chakula chao hao wakwe?
Jawabu:
الحمد لله رب العالمين، والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء وأمام المرسلين، نبينا محمد وآله وصحبه وسلم.
Bila shaka katika ambayo huimarisha msingi wa al-walaa wal-baraa ni Muislamu kuchukizwa na kila ambacho humchukiza ALLAAH tabaaraka wata’aalaa.
Na hawapishani Waislamu wawili kuwa jambo la Waislamu wawili kuishi kiunyumba bila ya ndoa jambo hilo linamghadhibisha ALLAAH na huwa na wivu kuona waja wake wanazini.
Amesema Mtume (Swalla LLAAHU ‘alayhi wasallam):
“يا أمة محمد ما من أحد أغير من الله -تعالى أن يزني عبده أو تزني أمته” متفق عليه
Enyi ummah wa Muhammad! Hakuna yeyote ambaye ana wivu kumshinda ALLAAH, pale anapozini Mja wake au kijakazi wake
Sasa ili kufikia hilo ni muhali kula chakula chao kwani kufanya hivyo ni kuonesha ridhaa juu ya maasi yao wayafanyao.
Na kuacha kula chakula chao huku ukiwa unawanasihi ni dalili ya wazi juu ya kuchukia matendo yao hayo hata kama ni wakwe zako.
والله ولي التوفيق
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 27/01/2017