Kula Kichinjwa Cha Mlevi


Swali.
Ukikaribishwa chakula na mtu ni waislam wote ila aliyechinja kuku anakunywa pombe unaweza kula hicho chakula?
www.duaatsalaftz.net ikilisherehesha swali ili lieleweke kwa Mwenye kujibu
Yani watu wafamilia wote ni waislamu wakamkaribisha mtu chakula na kukawa na kitoweo cha kuku. Ila mchinjaji wa kuku ni muislamu mnywa pombe, sasa ndio muulizaji auliza inajuzu kula kichinjwa hicho?
Jawabu:
الحمد لله رب العالمين ، والصلاة والسلام على رسول الله محمد بن عبد الله وآله وصحبه.
ALLAAH -‘Azza wajallah- ameharamisha pombe kwenye Qur’an na akatwambia ni katika matendo ya shetani tujiepushe nayo.
Na kumywa pombe ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.
Bali baadhi ya Wanazuoni wameliita dhambi hilo kuwa ni ummul-khabaaith mama wa mabaya yote.
Anaweza kunywa pombe akatukana, akazini na bintiye, akaua nk.
Na nadra kumpata mlevi anayeswali.
Na asiyeswali ni kafiri kwa kauli yenye nguvu miongoni mwa kauli za Wanazuoni.
Kwa ushahidi wa hadithi aliyoipokea Imaam Muslim (ALLAAH Amraham!) , kutoka kwa Jaabir Bin ‘Abdillaah (ALLAAH Amridhi!). Amesema Mtume (Swalla LLAAHU ‘alayhi wasallam):
“Baina ya Mtu kuingia kwenye ushirikina na ukafiri (mkubwa) ni kuacha kuswali”.
Hivyo haifai kula kichinjwa cha asiyeswali.
Na kuchinja ni ibada ni vyema isimamiwe na mtu mwema mchaji.
والله ولي التوفيق.
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 22/10/2016