Kumpa Talaka Mke Akiwa Katika Hedhi


Swali:
As salaamu Alaykum Warahmatullaahi Wabarakaatuhu!
swali liko hivi mwanamume amemuacha mke talaka rejea, akiwa katika hedhi, pasipo yeye kufahamu, na mwanamke hakua anajua kua kufanyika hilo ni kosa akaendelea kua eda. ikiwa eda imeshaisha anafahamu kumbe kufanyika hivyo ni haramu, mume nae anadai hakua akijua kua ni haram. sasa je kwa mujibu wa sheria hii inakua ni talaka? baarakallaahu fiikum.
Jawabu:
وعليكم السلام ورحمة الله وبركاته.
الحمد لله رب العالمين، والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء وإمام المرسلين، نبينا محمد وآله وصحبه وسلم.
Jumla ya kauli ni kuwa haifai kumuacha mwanamke akiwa kwenye hedhi au kwenye twahara ambayo amemuingilia ndani yake
Na hilo la kumtaliki mwanamke akiwa kwenye ada yake ya mwezi limehesabika kuwa ni jambo la kizushi katika Dini na kwenda kinyume na shari’ah ya ALLAAH (Sub-haanah!).
Pamoja kuna khilafu kuu ya Wanazuoni juu ya kupita au kutopita kwa talaka hiyo.
Jopo la welio wengi katika Wanazuoni wanaonelea kuwa talaka imepita na aliyeyafanya hayo anapata madhambi na ni juu yake kutubia kwa ALLAAH.
Na wako baadhi yao wanaoonelea kuwa talaka haipiti kama vile Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah na mwanafunzi wake Ibn Al-Qayyim (ALLAAH Awarham!).
Ama kwa mazingira ya suali lako kuwa huyo aliyeacha kwa sura hiyo ya kutojua kuwa mwenzake yupo katika ada yake mwezi basi hatochukuliwa kwa kile ambacho hajakidhamiria pamoja ya kuwa talaka hiyo imepita.
ALLAAH Anasema :
“وليس عليكم جناح فيما أخطأتم به ولكن ما تعمدت قلوبكم”
Na wala hamna dhambi (wala hatia) kwa yale mliyokosea kwa kutokujua lakini atakuchukulieni ALLAAH (kwa adhabu) kwa yale mliyoyadhamiria kwenye nyoyo zenu
Na amesema Ibn Kathiir (ALLAAH Yarham-hu!):
وإنما الإثم على من تعمد الباطل
Na hakika si jenginelo madhambi ni kwa yule ambaye amedhamiria batili
Ni wajibu kwa Waislamu kuwa makini katika masuala mazima ya kuwataliki wake zao na wachunge shari’ah ya Dini juu ya hilo na wasifanye mambo kwa kudhani bali wafanye kwa yakini.
والله ولي التوفيق
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 27/01/2017