Kuswali Msikiti Wenye Kaburi


Swali:
Ni ipi hukmu ya kuswali tahiyyat masjid katika msikiti ambao ndani / mbele yake kuna kaburi, umeingia kutokana na mnasaba. Mfano kwa Haruc n.k
Jawabu:
الحمد لله رب العالمين، والصلاة والسلام على رسول الله وآله وصحبه
وبعد.
Haifai kuswali tahiyyatul-masjid katika msikiti ambao una kaburi/makaburi , mbele yake au nyuma yake na pembizoni mwake muda wa kuwa ni katika kiwanja cha msikiti.
Kwa kuenea kwa hadithi iliyokataza jambo hilo.
Amesema Ibn Baaz (ALLAAH Amraham!):
“Kuswali kwenye makaburi swala yenye rukuu na sijda haifai.
Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amesema:
“ALLAAH Awalani mayahudi na manaswara, wameyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa ni Misikiti”.
Na kila kaburi litakaloswaliwa mbele yake litakuwa limefanywa msikiti hata kama halijajengewa jengo la Msikiti.
Na amesema Mtume (swalla LLaahu ‘alayhi wasallam):
“Eleweni kuwa waliopita kabla yenu walikuwa wakayajaalia makaburi ya Manabii wao na Wema wao kuwa ni Misikiti.
Zindukeni! Msiyafanye makaburi kuwa ni misikiti mimi nakukatazeni hilo”.
Na wala usighurike na kauli za watu kuwa Msikiti wa Madinah una makaburi ndani yake kwani asli yake ni kuwa makaburi yalikuwa ndani ya chumba cha Mama ‘Aaishah (ALLAH Amridhi!) ndani ya nyumba yake.
Hayakuingizwa makaburi ndani ya Msikiti ila mwaka wa themanini na nane tangu alipozikwa Mtume (swalla LLAAHU ‘alayhi wasallam) mwaka wa kumi na moja.
Na tukio la kuingizwa ndani ya msikiti makaburi hayo walilikataa Wanazuoni wa Madinah.
والله ولي التوفيق
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 24/10/2016