Malipo Ya Wale Ambao Mema Na Maovu Yao Ni Sawa


Swali:
Ni mahala gani au mafikio gani au malipo gani watakayolipwa watu ambao mema yao na maovu yao yatakuwa sawa. Barakallahu fikum.
Jawabu:
Wafiikum Baarakallaahu!
Aliulizwa swali kama hilo Mufti Ibn Baaz.
Akajibu (ALLAAH Amraham!):
“ALLAAH ni Mjuzi zaidi wa hilo, jambo lake lipo kwa ALLAAH -Subhaanah!- lakini ni lazima tukate kauli kuwa maishilio yake ni pepo.
Ama kuwa yeye ataadhibiwa au hatoadhibiwa hili lipo kwa ALLAAH -Subhaanah wata’aala!-.
Kwasababu mtu wa tawhiid ambaye mema yake na mabaya yake yapo sawa mwisho wake ni peponi.
Lakini huenda akasamehewa kwa fadhla za ALLAAH-Subhaanah!- (na Ihsani zake) na akaingia peponi mwanzoni (bila ya kuadhibiwa).
Na inawezeka akaadhibiwa katika moto kwa makosa yake ambayo hakutubia.
Hivyo atakuwa chini ya matashi ya ALLAH-‘Azza wajalla!-…”
من موقعه -رحمه الله-
والله ولي التوفيق
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 22/10/2016