Mwanamke Kusoma Quran, Kukaa Msikitini Na Kusikiza Darsa Wakati Wa Hedhi


Swali:
kuna jambo linanitatiza sana je mwanamke akiwa katika haydhi inajuzu kwake kusoma quran,kukaa msikini na kusikiliza darasa naomba unijibu kwa dalili nipate jibu sahihi?
Jawabu:
الحمد لله رب العالمين ، والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء وأمام المرسلين وبعد
Bila shaka halali ni ile iliyohalalishwa na Shari’ah na haramu pia ni ile iliyoharamishwa na Shari’ah.
Ama kuhusu suala la mwanamke aliye katika ada yake kuruhusika au kutoruhusika kusoma Qur’an ni jambo ambalo lina khilafu mbele ya Wanazuoni wetu wa Ahlus-Sunnah (ALLAAH Awarhamu waliotangulia na Awahifadhi waliosalia!).
Baina ya wenye kusema haifai ila kwa dharura mfano wa kusoma Qur’an wakati wa usaili au mtihani shuleni na mfano wa hilo.
Na waliosema hakuna katazo lolote Kishari’ah lililokuja kukataza hayo, na mambo yanakwenda kwa dalili.
Ama dalili ambazo wamezitumia wale wanaokataza suala hilo katika Wanazuoni zimejadiliwa na Wanazuoni wanaokwenda kinyume na rai hiyo.
Katika waliyoyasema ni kuwa hadithi inayomkataza mwanamke mwenye hedhi/nifasi / janaba
Asishike chochote katika Qur’an ni hadithi Dhaifu.
Ama ayah isemayo
“Hauguswi ila na waliotwaharishwa” al-waaqi’ah aya ya 79.
Wamesema ayah hiyo haina mnasaba na kukatazwa mwenye hedhi wala nifasi.
Ayah huwazungumza Malaaikah (‘Alayhimus – Salaam!), na lawhil-mahfuudh.
Kwa ujumla hakuna dalili sahihi iliyo sarihi (wazi) inayomkataza mwenye hedhi kuisoma au kuishika Qur’an.
Bali imesihi Hadithi kuwa Mtume (Swalla LLAAHU ‘alayhi wasallam) alimwambia Mama ‘Aaishah ALLAAH Amridhi baada ya kuingia kwenye mzunguko wake wa Mwezi akiwa katika ibada ya hija:
“Yafanye yote yafanwayo na mwenye kuhiji ila tu usitufu kwenye ka’bah”.
Na wamekubaliana Waislam kuwa miongoni mwa yafanywayo na mahuhaji ni kusoma Qur’an.
والله ولي التوفيق
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 08/11/2016