NA KATIKA UWONGO WA HALALI NI MUME KUMDANGANYA MKE ( AU MKE KUMDANGANYA MUME )


 https://t.me/duaatsalaftz

Amepokea Imam Muslim (Allaah amraham) , kutoka kwa Kulthuum bin ‘Uqbah bin Abiy Mu’ayt (Allaah amridhie) , amesema:

((لم أسمع النبي صلى الله عليه وسلم ، يرخص في شيئ من الكذب إلا في ثلاث ، الحرب ، والإصلاح بين الناس ، وحديث الرجل امراته والمراة زوجها))

“Sijawahi kumsikia Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) Akiruhusu aina yoyote ya kuongopa ila katika sehemu tatu.

1. Kwenye vita.
2. Kusuluhisha baina ya watu.
3. Maongezi ya mtu kwa mkewe na mke kwa mumewe”.

Amesema Ibn Baaz (Allaah amraham) katika kuitolea ufafanuzi hii hadithi:

“Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) amemruhusu mwanamme kumdanganya mkewe , na mke kumdanganya mumewe pale utakapokuwa (uongo huo) una maslahi na haumdhuru yeyote. Bali unapokuwa unanufaisha wala haudhuru.

Kama vile atakampomdanganya (mke) kwa maslahi yanayofungamana na yeye au watu wake (mume huyo) , pasi na kudhurika yeyote. Uongo kama huu ni mzuri hauna ubaya.

Mathalan mke aseme:

“Hakika ndugu zako wanakupenda sana , na wanakusifia (maashallaah!) ,na wanapenda kukuona ukiendelea na tabia ya ukweli katika maongezi yako na mwenye maongezi mazuri kwao, na wanasifia zile huduma zako kwao. Lengo (la kumueleza hilo) ni kumpa moyo. Na mfano wa haya ayaseme mume kumwambia mke”.

Kwa haya maelezo ya Sheikh bin Baaz (Allaah amraham) , ameungana na wenzake waliokataza uongo wa kudanganya kwa uwazi kabisa , Bali ameruhusu uongo aina ya tawriyah , nao ni kukusudia mzungumzaji katika mazungumzo yake makusudio yaliyo sahihi ambayo si uongo kiupande wake (kwamba hivyo ndivyo mtu anavyotakiwa awe) japo kwa upande wa yule anayeambiwa ni uongo kwa mujibu wa dhahiri ya yale maneno.

Mfano uongo (aina ya Tawriyah/Ma’aariidh) wa Nabii Ibraahiim (‘alayhis-salaam) alipomwambia yule mfalme dhalimu ambaye alikuwa akichukuwa warembo katika wake za watu , ila ukisema kuwa uliye naye ni dada yako hamchukui.

Akasema Ibraahiim (‘alayhis-Salam) kumwambia Saaarrah.

“Akikuuliza huyu dhalimu kuhusu (mahusiano ya Mimi na wewe) basi mwambie wewe ni Dada yangu , kwani akijua kuwa wewe ni mke wangu atanipokonya”.

Akiwa anakusudia ni dada katika Iymaan wakati huo huo ni mkewe wa halali. Akanusurika MKEWE kutokana na vitimbi vya yule mfalme dhalimu. Na hadithi ameitaja Bukhariy na Muslim.

Na mfano wa hilo kwa Mtume wetu Muhammad (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) , ni riwaya aliyoitaja Ibn Is-haaq katika siyrah:

Ni pale alipokuwa na baadhi ya Maswahaba zake akakutana na mzee mmoja akamuulizia juu ya msafara wa maquraysh ukiongozwa na Abuu Sufyaan kabla ya kusilimu kwake (Allaah amridhie) , kisha yule mzee akamuuliza Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) ,

ممن أنتم؟

“Mmetokana na nani nyie?”.

Akajibu:

من ماء

“tumetokana na maai”

Hapa kwa haraka alielewa yule mzee kuwa kuna mji unaitwa maai, ndio maana akajiuliza maai ya misri au ya wapi? lakini kusudio la Mtume (swalla Llaahu ‘alayhi wasallam) ni kuwa wameumbwa kwa maji ya manii , kama alivyosema Allaah katika suuratul-Mursalaat:

أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ

“Hivi hatukukuumbeni kutokana na maai (maji) yaliyo dhalili?”.

Pia ametaja Shaykh Al-Shanqiitwiy , kuwa mmoja katika mataabiina ambaye ni Ibraahiim Al-Nakha’iyy (Allaah Amraham) , alikuwa ni kijakazi wake , ambaye wanapokuja watu waovu nyumbani kwa huyu Imam na wakamuulizia , yeye (kijakazi) huko ndani alipo anachora duara ardhini Kisha anamjibu kwa sauti anayemuuliza Imam:

“Wallaah! Imam hayumo humu ndani”.

Lakini yeye anakusudia hayupo ndani ya duara alilochora.

Kwa hayo maelezo tunapata taswira kuwa uongo ulioruhusiwa si ule uongo wa kudanganya moja kwa moja Bali ni ule ambao una sura ya ukweli katika upande fulani , na huutamka mtu kwa mazingira fulani ya kudharurika na wala haipendezi pia mtu kuufanya kuwa ndio maisha yake. Lengo la kuruhusika ni kuimarisha ndoa na kutengeneza tabia njema kwa mke.

Na haya ndiyo makusudio yake.

قال النووي رحمه الله في “شرح مسلم

Amesema Imam Nawawiy (Allaah amraham) katika Sharh yake kwa swahiih ya Muslim:

” وَأَمَّا كَذِبه لِزَوْجَتِهِ وَكَذِبهَا لَهُ

Ama mume kumdanganya kwake mke wake, na Mke kumdanganya mume,

فَالْمُرَاد بِهِ فِي إِظْهَار الْوُدّ

Kusudio lake ni katika hali ya kudhihirisha mapenzi (pendo tu , kama vile kumwambia mfano wako halijawahi kuona jicho langu ,mfano wako wameshindwa wanawake kumzaa)

وَالْوَعْد بِمَا لَا يَلْزَم

Na ahadi (kumuahidi) kwa yale yasiyo ya lazima, (kama vile kumwambia mathalan tutachoma mishikaki siku moja)

وَنَحْو ذَلِكَ ؛

Na mfano Wa hayo,

فَأَمَّا الْمُخَادَعَة فِي مَنْع مَا عَلَيْهِ أَوْ عَلَيْهَا

Ama kumhadaa katika hali ya kutaka kumnyima haki yake (Mke/mume),

أَوْ أَخْذ مَا لَيْسَ لَهُ أَوْ لَهَا فَهُوَ حَرَام بِإِجْمَاعِ الْمُسْلِمِينَ

Au kwa lengo la kutaka kuchukua kisichokuwa chake (mke /mume), jambo hili ni haramu kwa makubaliano ya waislam (kama vile mathalan ukamdanganya ili umtapeli ali yake nk.)

Na mfano wa hayo amesema Al-Khattwabiy (Allaah Amraham);

“فأما كذب الرجل زوجته فهو أن يعيدها ويمنيها ويظهر لها من المحبة أكثر مما في نفسه يستديم بذلك محبتها ويستصلح به خلقها”

“Ama suala la Mume kumdanganya mkewe ni yake ni kule kumpa matumaini na kumdhihirishia mapenzi zaidi ya mapenzi yaliyomo nafsi ni mwake (mwanamme huyo) , lengo lake ni kudumisha mapenzi ya mkewe (kwake) , na kumtengeneza mke kitabia”.

Haya yote ukiyasoma utaona lengo ni kuimarisha ndoa na kuidumisha katika kipindi ambacho usipofanya hivyo madhara yake ni makubwa ambayo huenda yakapelekea kuvunjika kwa ndoa au kuzalisha migogoro isiyohimidiwa mwisho wake.

Haifai kulifanya hili kuwa ndio dezo lake mtu , au akalifanya hili kuwa ni daydanah yake kila uchao.

Na haifai kusema uongo wa dhahiri kama wanavyoruhusu hilo baadhi ya Masheikh , Bali ni kutumia tawriyah au ma’aariidh kama tulivyotoa mifano yake.

 

وكتب/ أبو أيمن الشيرازي -كان الله له في الدارين

. ▪•┈•◈◉✹❒📚❒✹◉◈•┈•▪

     https://t.me/duaatsalaftz

​​​​​​​​​​​​tembelea Channel yetu ya telegram ili kupata faida zaidi ​​​​​​​​​kwa kupitia kiunganishi kilichowekwa
​​​

​​
​​​جزى الله خيرا كل من قرأها وساعدنا على نشرها