Ni Katika Mazingira Gani Yafaa Kula Kilichoharamishwa?


Swali:
Assalaam alaikum warahmatullah wabarakatuh , jee ya faa kula chumo la haramu katika mazingira gani ?
Jawabu:
Wa alaykumus salaam warahmatullaah wabarakaaatuh:
Haramu ni aliyoiharamisha ALLAAH (subhaanah).
Na ALLAAH ametutaka tule vilivyo vizuri.
Ama ikitokea mazingira tata ambayo vya halali hakuna na mtu anaweza akafa kwa sababu ya njaa basi hapo amedharurika kula nguruwe ambaye ni haramu kabla ya hapo.
Japo ulaji wa kudharurika hauwi sawa na ulaji wa kuburudika.
Utakula bila ya chumvi wala kachumbari.
Utakula kwa kiasi kidogo tu cha kuweza kuinua uti wako wa mgongo ili utembee mbele upate chakula cha halali.
Na katika kanuni
” DHARURA HUKADIRIWA KWA MAKADIRIO YAKE”
والله ولي التوفيق
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 09/12/2016