Ni Lazima Khutbah Mbili Katika Swala Ya Ijumaa


Swali:
بسم الله الرحمن الرحيم
السلام عليكم ورحمت الله وبركاته
Mimi swali langu ni kwamba, nilishaawahi kuswali swala ya ijumaa msikiti mmoja hapa mjini dar es salaamu, khatwib akakhutubu khutba moja tu wakati anashuka mimbari maamuma wakamkumbusha kuwa umekhutubu khutba moja tu, khatwibu akasema inatosha. Pakakimiwa kisha tukaswali. Vipi hili linajuzu? Kama haijuzu vipi hukmu ya swala yetu?
Jawabu:
وعليكم السلام ورحمة الله وبركاته.
الحمد لله رب العالمين ، والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء والمرسلين وآله وصحبه
وبعد.
Swali kama hili aliulizwa Al-Imaam Ibn Baaz (ALLAAH Amraham!), akasema:
“Swala si sahihi, na ni wajibu wake arudie kutoa khutba ya pili kisha airudie swala. Lazima khutba mbili zipatikane kama alivyofanya Mtume (swalla LLAAHU ‘alayhi wasallam).
Na khutba mbili ni sharti ya kuswihi kwa swala. Hili ndilo jambo la sahihi.
Kwahiyo ni wajibu kwa mtu huyu airudie swala yeye na wenzake waswali adhuhri. Na ijumaa ijayo lazma wakhutubu khutba mbili..”. (fataawa).
والله ولي التوفيق
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 09/12/2016