Nini Ufanye Unaposahau Nguzo Au Wajibu Ktk Swala


Swali:
Assalam alaykum warahmatullah swali langu je ukikosea katika nguzo za swala mwisho wa swala utasujudu sijda mbili pia ukiacha wajibu wa swala pia ukasujudu sijda hizo mbili?.
ningependa kuwaomba mumtadhaharishe shekh jina lake Dimoso anaeneza sana cd zake na zinauzwa huyi ni jaahil msikilizeni
jawabu:
الحمد لله والصلاة والسلام على رسول الله محمد بن عبدالله وآله وصبحه
وبعد:
Ukikosea katika nguzo za swala utatakiwa uzilete kisha utasujudu sijda ya kusahau.
Kadhaalika ukiacha wajibu miongoni mwa waajibaaatis-swalaaah utasujudu kabla ya kutoa salamu sijdah ya kusahau bila ya kuileta hiyo waajib.
Na sijdatus-sahawi imewekwa kwa moja miongoni mwa mambo matatu makuu.
1. Kuzidisha
2. Kusahau
3. Kuwa na mashaka

Ama kuhusu ombi lako la kumtahadharisha bwana tajwa hapo juu, kiukweli sisi hatumjui.
Pamoja ya kuwa tunawatahadharisha mashabaab wa sunnah na wazee wao kutokana na kuwategea sikio walinganizi wa bid’ah kwa sampuli zao zote.
Ima wawe ni watu wa mawlid, khitmah, talakini, watu wa visa, mahajaawirah, mahizbiy, wanaharakati na sakanaati , mashia , masufi , maibadhi na wengineo wote.
والله ولي التوفيق
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 09/12/2016