Ubaya wa Riyaa katika matendo


Swali :
Assalamu Aleykum warahmatullah Wabarakaatuh
Je mtu anapomswalia mtume Swalla llahu alayhi wasallam kwa ria anapata thawabu?
Jibu :

وعليكم السلام ورحمة الله وبركاته

الحمد لله رب العالمين والصلاة والسلام على رسول الله صلى الله عليه وسلم

Ndugu muulizaji:
Tambua yakwamba amepata khasara yule ambaye atafanya matendo mema kwa riyaa
Yaani hatoambuliachochote siku ya qiyamah kwa matendo yake hayo.

قال الشيخ محمد أمان الجامي رحمه الله

Amesema kwalo ( riyaa ) Sheikh Muhamad Amaani Aljaamiy , Allaah amrehemu.

قد يكون الإنسان : ينفق نفقات عظيمة ويتعلم فيعلم ويجاهد فيقتل

Mwanaadamu huenda akawa anatoa Mali ( kwa wingi mno ) zenye hadhi,
Na akawa anasoma na huwa mwenye kuelewa ( kile anacho kisoma ),
Na anapigana jihadi katika njia ya Allah Tabaaraka Wata’aala na anauliwa ( huku akiwa katika jihaadi )

كل ذلك إذا دخله الرياء ضاع وبطل

Yote hayo ( ambayo mwanaadamu anayafanya ) Endapo yataingiliwa ndani yake na RIYAA ( basi ) huwa yanapotea na yanabatilika ( yaani hakuna malipo ndani yake )
Hivyo ndugu muulizaji riyaa haichanganyiki na matendo yeyote na pindi inapoingia riyaa katika matendo basi matendo hufisidika ( yanabatilika ) kama unavyobatilika udhu pindi unapooatwa na hadathi.
Na Allah Tabaaraka Wata’aala ni mjuzi zaidi.
Mhusika : Sheikh Muhammad Amaani Al-jaamiy
Marejeo : qurratu ‘uyuunul muwahidiin (Uk. 20)
Mfasiri : duaatsalaftz.net
Imehaririwa : 06′ J-Uwlaa/143