Urahisi na Ulaini ni sifa ya Muislamu


قال  العلامة  ابن  عثيمين  رحمه الله

وظيفة  المسلم  مع  إخوانه

أن يكون  هينا  لينا  بالقول  وبالفعل

لأن هذا مما يوجب  المودة  والألفة بين الناس

{شرح  رياض  الصالحين  2/544}

 

Amesema Mwanachuoni Ibn Uthaymiin Allah Amrehemu:

Kazi ya muislamu akiwa pamoja na ndudu zake {waislamu},

Ni awe mrahisi{mwepesi} na  mlaini kwa maneno na matendo,

  Kwa sababu hii ni miongoni mwa mambo yanayoleta mapenzi na uzoefu baina ya watu.

Rejea:

Sherehe ya Kitabu Riyaadh Asiswalihiin [2/544]

MAELEZO:

Hali hii ya kuwa mlaini na mwepesi kwa waislamu pia inatofautiana kwani:-

Haiwi sawa hali yako utakapokuwa umekutana na Salifiyyu {Ahlu-Sunnah wal-jamaa} na pindi unapokutana na Mub-tadi3,Mtu wa matamanio au talbiis..

Lakini ni ajabu sana kuona baadhi ya watu wamekuwa wakiufanyia kazi msingi huu kinyume .

نسأل الله السلامة والعافية