Vipi Mtu Apate Dhambi Kwa Kuacha Aliyoharamisha Allah?


Swali:
kuna mashaikh wanasema mtu atapata madhambi akiacha kusoma kwa riba chuo kikuu mf. hapa TANZANIA ili usome chuo kikuu lazima uombe mkopo ndpo uweze kusoma chuo je kuna dalili au kuna ikhtilaf juu ya hilo?
na je mchanganyiko baina ya mabanat na wanaume ktk mashule na vyuo kuna dharura yoyote ?
Jawabu:
الحمد لله رب العالمين ، والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء وإمام المرسلين
وبعد
Hao ni walinganizi wa batili.
Tangu lini mtu akiacha haramu kwa lengo la kuitakasa Dini yake anapata dhambi!?
Huku ni kugeuza vipimo.
Allaah ameiharamisha riba kwenye kitabu chake.
Na Mtume (swalla LLAAHU ‘alayhi wasallam) amekataza riba.
Na akatwambia kuwa mla riba ni maluuni na mwakilishi wake na mashahidi wake.
Na wala hakuna udharura wa kuchukua riba.
Ikiwa hana budi mtu kusoma na auze shamba lake au akope kwa mtu mkopo wa halali ambao hauna riba.
Jambo la riba ni khatari kwa Muislam.
Riba ya mwisho kiudogo ambayo hakuna aijuaye zaidi ya ALLAAH ni sawa na mtu kuzini na mama yake hadharani.
والله ولي التوفيق
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 09/12/2016