Yafaa Kuoa Ndoa Mbili Ndani Ya Wiki Moja?


Swali:
vp kuoa ndoa mbil ndani ya wiki moja ktkt muda tofaut?
Jawabu:
الحمد لله رب العالمين ، والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء وإمام المرسلين
وبعد.
Kuoa ndoa mbili ndani ya wiki moja hakuna ubaya ikiwa hilo halitoharibu fungate ya mke mmoja miongoni mwa hao.
Mfano umeoa mjane ukakaa kwake fungate siku tatu, na baada ya siku hiyo ukaoa tena mjane ama bikra ukakaa naye siku saba.
Ama kuoa mwanamke ndani ya wiki hiyo hiyo kabla ya kuisha fungate ukaoa mwengine. Au kuoa mjane au bikra siku moja ni jambo la makruuh kama walivyopitisha hilo baadhi ya hanaabilah kama vile Al-Imaam Al-Buhuutiy kwenye “Kashaaf” na Ibn Qudaamah “Al-Mughniy”.
Ni vyema kutofanya hivyo kwani kusubiri fungate ya mmoja wao kumalizika ni jambo la awlaa.
والله أعلم
Muhusika: duaatsalaftz
Chanzo: www.duaatsalaftz.net
Imehaririwa: 09/12/2016